Moja ya kitu cha kutia moyo tukionacho katika kazi zetu, ni jinsi wanawake wengi wanavyowasiliana nasi, wanauliza jinsi watakavyoweza kutusaidia. Huu ni mwongozo wa vitu unavyoweza kufanya kusaidia Wanawake Pamoja katika kazi zetu, na jinsi utakakavyosaidia kuboresha maisha ya wanawake katika jamii yako na katika Tanzania:

 

Sambaza Ujumbe

 

Wanawake wengi wanaonyanyasika hawajui kama wana haki, na hakika hawajui waende wapi kupata msaada. Kwa kueneza ujumbe kuhusu haki za wanawake na wapi  pa kupata msaada, unaweza kuokoa maisha

Taarifa hizi zinaweza kusambazwa kupitia: Sehemu ya kupata msaada. 

Kutoa taarifa kwa mdomo- Zungumza na rafiki yako masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, wote wanaume na wanawake. Wajue msimamo wako, na kusambaza taarifa kuhusu wapi unapoweza kupata msaada aina mbalimbali (Unganisha kwa Facebook Sehemu ya kupata msaada).

 

Ingilia kati

 Tumeshazoea kuukubali unyanyasi wa kijinsia,Tunasema kwamba “Hili ni jambo binafsi” au “Hili ni jambo gumu kujishughulisha nalo” au “haiwezekani kubadilisha hali hii”.Lakini unaweza kuleta mabadiliko” Kama unamwona mwanaume anamnyanyasa mpenzi wake,h aya ni mapendekezo ya jinsi unavyoweza kuingilia kati:

  • Nenda kazungumze na mwanaume, na kumtuliza au kuingilia na kumfanya mwanamke apate upenyo wa kutoroka
  • Hata kama huwezi kumudu kuingilia kati wewe mwenyewe, mtume mtu mwingine,labda mwanaume
  • Piga simu polisi simu namba 112. Unaweza kuomba msaada kutoka Dawati la kijinsia
  • Mtake mwenyekiti wa mtaa kuingilia kati. Unyanyasaji majumbani ni kosa la Jinai na linapaswa lishughulikiwe ipasavyo. Analazimika kuingilia kati.
  • Wajulishe familia, majirani na marafiki kuhusu haki za wanawake na washawishi walishughulikie pamoja na wewe.

 

Changia

Wanawake Pamoja inategemea michango yako. Kupitia michango yako, tutaweza kuwafikia wanawake wa rika zote, nchini kote, na kuweza kuleta tofauti kwa maisha ya wengi. Tafadhali changia leo kutusaidia kufanya kazi hii muhimu! Bofya hapa (Kiunganishi) link coming soon.  

 

Jinsi ya kuwa mfanyakazi wa kujitolea (Voluntia)

Mara nyingi tunahitaji watu wa kujitolea(voluntia) wenye ujuzi mbalimbali. Nafasi zetu za kujitolea zote tunaziweka kwenye UKURASA HUU(Kiunganishi na ukurasa) ambapo unaweza kupata kujua jinsi ya kusaidia. Ukurasa huu unasahihishwa(updated) kila mara.