Kuhusu taasisi yetu

Wanawake Pamoja ni taasisi mpya kabisa inayojihusisha na haki za wanawake. Ukurasa wetu wa Facebook Wanawakekaitika harakati za kupinga ukatili wa kijinsia ulianzishwa tarehe 8 mwezi wa tano mwaka 2016, na taasisi yetu inasajiliwa mwezi wa Desemba mwaka 2016.

 

Maono yetu


Wanawake Pamoja inawaleta pamoja wanawake kumaliza tatizo unanyanyasaji kwa kusambaza taarifa, kuwawezesha wanawake na kuwapa vifaa, ujuzi, elimu na kujithamini na kutengeneza maisha bora ya baadaye kwa wao wenyewe na watoto wao.

 

Malengo yetu

 

Wanawake pamoja inalenga kuona nchi yenye jinsia zote zinaheshimiwa katika kila nyumba yenye familia, kila mahali pa kazi na katika jamii zote. Kuona jamii inayoheshimu haki za wanawake katika nyanza zote za jamii, uchumi na katika siasa.