Wanawake Pamoja ni taasisi isiyo na faida inayojishughulisha na haki za wanawake katika Tanzania.Unyanyasaji wa kijinsia ni tatizo lililosambaa kote nchini kwetu ,ambapo wanawake na wasichana linawakumba kila siku.Matatizo haya yanahitaji kutatuliwa kwa njia mbalimbali ili kuboresha hali ya mwanamke kijamii,kiuchumi na kisiasa.

Hivi ndivyo tunavyofanya kazi:

Mitandao ya kijamii

Ukurasa wetu wa Facebook Wanawake katika harakati za kupinga ukatili wa kijinsia Upo hai kubadilishana taarifa kuhusu haki za wanawake na masuala yanayowahusu wanawake.Kupitia njia hii tumeweza kuwafikia wanawake nchi nzima,wa rika zote

Hapa ,wanawake wanaweza kupata taarifa ,kubadilishana taarifa na mawazo,na kuwasiliana nasi kama wanahitaji msaada au wanamjua mtu anayehitaji msaada. Pia tumeona kwamba watu wengi wanawasiliana nasi kwasababu wanataka kusaidia,na wanajihusisha na kazi zetu kwa kutembelea UKURASA HUU (small changes to the text).

Msaasa/ushauri nasaha

Tunatoa msaada binafsi kwa wanawake kukwepa unyanyasaji wa kijinsia,na tunaweza kupatikana kwenye simu au kwenye ukurasa wetu wa facebook.Wahudumu wetu na wafanyakazi wa kujitolea wanasaidia wanawake kuwasiliana na watu muafaka,kwa mfano polisi,msaada wa kisheria,msaada wa matibabu na malazi.

Kituo cha uwezehaji

Tupo kwenye hatua za awali za kuanzisha kituo cha uwezeshaji kwa wanawake. Kituo kitatoa huduma za malazi kwa wanawake na watoto waliopatwa na matatizo ya unyanyasaji wa kijinsia,pamoja na msaada, ushauri nasaha,mafunzo ya ujuzi na jinsi ya kujilinda.